Samia aahidi Zanzibar yenye neema tele
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi mambo matano atakayoyatekeleza kwa ushirikiano na mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Dk Hussein Mwinyi endapo watapata ridhaa ya kuongoza nchi.
Akizungumza na wananchi wa majimbo ya uchaguzi ya Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, Samia amesema ahadi yake ni kufanikisha yote waliyoelekezwa kwenye ilani ya uchaguzi ya 2025- 2030 kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar zinathamini sana utekelezaji wa ahadi zinazotolewa na chama chetu. Tumefanya tathmini ilani iliyopita, tumefanya vizuri katika kuitekele- za, kwa ilani tunayoinadi sasa hivi, mambo mengi na makubwa zaidi yanakwenda kufanyika,” amesema.
SOMA: Samia ajivunia makubwa ya CCM kwa nchi
Akitaja mambo hayo, amesema la kwanza ni kuulinda muungano kwa nguvu zote, kwani umekuwa na faida kwa pande zote mbili (Bara na Zanzibar).
“La pili, tutakalofanyia kazi kwa nguvu zote ni maendeleo jumuishi yanayo muhusu kila mtu kwenye elimu, afya, maji na umeme. Tutafanya kazi kwa pamoja, kuhakikisha huduma za jamii zinamfikia kila mtu,” amesema.
Amesema anatambua kwa sasa kuna changamoto ya umeme Zanzibar na kuwa- hakikishia yeye (Samia) na Dk Mwinyi wamesimama imara kwenye hilo na lengo lao miaka mitano ijayo, Zan- zibar haitakuwa na shida ya umeme.
Jambo la tatu aliloahidi ni uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kusaidiwa kupatiwa mitaji na fursa kwa vijana, kuwawezesha kujiajiri na kuajiriwa:“Lakini kubwa waweze kuendesha maisha yao,” alisema.
Aliongeza: “Lingine ni kukuza uchumi mkubwa, pande hizi mbili (Bara na Zanzibar) zinafanya kazi kwa pamoja kuukuza uchumi. Tunafanya kazi kuhakikisha vichocheo vya uchumi tumeviimarisha kama usafiri wa maji, anga, maana tukirahi- sisha usafiri, tunarahisisha biashara na uchumi wa nchi yetu,” amesema.
“Lakini pia, tutafanyia kazi sekta ya uzalishaji, uchumi wa buluu, utalii, viwanda na biashara. Mafuta, gesi, uvuvi wa bahari kuu ni maeneo yanatupa mwanga kwa ajili ya vijana wetu.”
Aidha, kwenye utawala bora aliahidi kuwa na katiba mpya, kwani ni takwa la watu kutoka vyama vya upinzani na hata ndani ya chama chake.
Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29 na hakuna lolote litakalowakuta, kwani nchi iko salama.
“Waliokuwa wakisema Oktoba tuna jambo letu, sasa jambo lipo uwanjani, wavae njuga wakatekeleze… hatuna budi kuchagua Chama Cha Mapinduzi bila kupepesa macho. Nendeni mkapige kura bila wasiwasi wowote, wito wangu kwa kila aliyeji- andikisha kwenye daftari la mpigakura, aende akapige kura,” alisema.
Dk Mwinyi amesema kwa kampeni walizofanya, anaamini chama chake kitapata ushindi wa kishindo.
“Kampeni tumezifanya kwa ustaarabu mkubwa, watu wengi na makundi maalumu tuna imani kote huko tulipopita wananchi watatuchagua kwa kishindo, nasi hatuna sababu ya kutoamini hilo. Kampeni ni suala moja na kupiga kura ni suala lingine, niwaombe wananchi mjitokeze kupiga kura. Nimuombee kura
Samia, mimi mwenyewe na wawakilishi,” amesema.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com