Sekou Toure yapongeza mafanikio ya sekta ya afya

MWANZA: HOSPITALI ya Rufaa ya mkoa Sekou toure imempongeza Rais wa Jamuhuri y Muungano Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Hospitali hiyo katika vifaa tiba na miundo mbinu .

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure, Bahati Msaki wakati wa Tamasha la Mbio Pole na kupongeza mafanikio ya sekta ya afya liliofanyika katika viwanja vya Sekou Toure mkoani Mwanza

Msaki amesema tokea Rais Samia aingie madarakani mpaka sasa, Hospital yao ilipokea mtambo wa kuzalishia hewa tiba kwajili ya kutengeneza hewa tiba na mtambo huo tayari umesimikwa na ulianza kuzalisha hewa tiba.

Amesema uwepo wa mtambo huo umesaidia kuokoa shilingi milioni 54 zilizokuwa zikitumika kununua vifaa hewa tiba kwa wazabuni.

Amesema hospitali yao inatoa huduma ya M-mama tokea Mei 2023 na mpaka sasa wagonjwa 10743 wamepata huduma kwa mchanganuo wa wakina mama 8193, watoto 2537 na mama na mtoto kwa pamoja 13.

Katika miundo mbinu,Msaki amesema Serikali iliboresha miundo mbinu ya majengo mbalimbali ikiwemo jengo la huduma za ufuaji na ujenzi wa jengo ya kusimika kiteketeza taka cha kisasa.

Amesema katika mwaka huu wa fedha 2025/2026 hospitali yao inategemea kuanza ujenzi wa jengo jipya la kisasa la wagonjwa wa dharura na ajali(EMD), OPD na wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu(ICU).

Akielezea zaidi kuhusu ujenzi huo, Msaki amesema jengo hilo litakuwa na ghorofa tisa na tayari wameshatenga shilingi bilioni 5 kwajili ya ujenzi wa jengo hilo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button