Mnyama kumaliza kazi kwa Mkapa leo

DAR ES SALAAM: Klabu ya Simba SC inaingia dimbani kwenye mchezo wa marudiano wa kufuzu makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nsingizini FC kutoka Eswatini, mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam leo.
Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na faida ya ushindi wa mabao 3–0 iliyoupata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini, hivyo inahitaji sare tu au kuepuka kipigo cha mabao manne ili kufuzu makundi.



