RC Mtanda: Wananchi wawe huru kufanya shughuli zao

MWANZA: MKUU wa Mkoa wa Mwanza, said Mtanda, ameondoa agizo la wananchi kuhakikisha wapo nyumbani saa 12 jioni, kwa sababu za kiusalama kufuatia vurugu zilizojitokeza hivi karibuni.

Hata hivyo, amefafanua kwamba haikua amri kama ilivyotafsiriwa, ikizingatia yeye hana mamlaka ya kufanya hivyo, ispokuwa Inspekta Generali wa Polisi (IJP) pekee.

RC Mtanda amesema hayo leo Novemba 5, 2025 na kuongeza kuwa: “Na katika matamko yangu yote nilikua nasema nashauri kwamba ifikapo saa 12 kama mtu hana jambo la lazima arejee nyumbani, ingawaje anayeshauriwa ana hiari ya kukubali au kukataa”.

“Kwahiyo mkoa huu hatukuweka katazo, ila tuliweka angalizo. Na baada ya malekezo ya mheshimiwa Rais, watu wawe huru kuendesha shughuli zao,” amefafanua.

Upande wa baa, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imekubaliana ziwe wazi hadi saa 4 usiku, wakati tathmini ikiendelea kufanyika, na baadaye watarudishiwa muda wao uleule wa kufunga saa 6 usiku.

Ni kwa sababu meneo ya baa watu wakishapata vinywaji wanaweza kuanzisha vurugu na wengine kutumia fursa hiyo kufanya mambo mengine hatarishi, hivyo ikiwa bado ni ndani ya muda uliotolewa kwa sasa ni rahisi mamlaka husika kuokoa wale wanaostahili kwani serikali haitaki mtu apoteze maisha.

“Kwahiyo wananchi wa Mwanza wawe huru kutembea,” amesistiza

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button