Sillo achaguliwa kumsaidia Zungu

BUNGE la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limempitisha kwa asilimia 100 Mbunge wa Babati Vijijini, Daniel Sillo awe Naibu Spika. Sillo alikuwa ni mgombea pekee wa nafasi hiyo na alipata kura zote 371 zilizopigwa bungeni jijini Dodoma.

Kabla na baada ya uchaguzi, Sillo ameahidi kushirikiana kwa karibu na Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kusimamia shughuli za Bunge. Aidha, ameahidi kulinda Katiba ya Tanzania na kufuata Kanuni za Bunge la Taifa ambazo ndizo zinazoongoza shughuli za Bunge. “Ninatambua kwamba tupo hapa kwa niaba ya wananchi. Nitasimamia mijadala yote nitakayopangiwa na Spika kwa manufaa mapana ya Watanzania,” alisema Sillo mara baada ya kula kiapo.

Sillo amewashukuru wabunge kwa imani yao kwake na akahimiza ushirikiano na Spika, akiahidi kutoa ushauri kwa uadilifu kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote. Safari ya kisiasa ya Sillo ilianza mwaka 2015 alipojitokeza kugombea ubunge kwa mara ya kwanza lakini hakufanikiwa. Sillo aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2020 na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika Bunge la 12.

Nafasi hiyo ilimpa fursa ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge, nafasi aliyochaguliwa Aprili 4, 2023, kiti ambacho kiliachwa na Zungu baada ya kuchaguliwa kuwa Naibu Spika. Baadaye, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. SOMA: Zungu ndiye Spika wa Bunge

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button