Wizara ya Vijana inakuja!

DODOMA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Sita imepanga kuanzisha Wizara ya Vijana itakayoshughulikia kwa ukaribu mambo yote yanayowahusu vijana nchini.

Akizungumza Novemba 14, 2025 wakati akifungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Dodoma, Dk Samia amesema mbali na kuanzisha wizara hiyo pia anatarajia kuwa na washauri wa Rais watakaomshauri kuhusu mambo ya vijana ikiwemo changamoto zao.

“Mimi na wenzangu katika Serikali tumefikiria kuwa na wizara kamili itakayoshughulikia Mambo ya Vijana”. Tumeamua kuwa na wizara kamili badala ya kuwa na idara kwenye wizara yenye mambo mengi” amesema Dk Samia na kuongeza kuwa

“Vilevile nafikiria kuwa na washauri wa masuala ya vijana ndani ya Ofisi ya Rais,” amesema Rais Samia.

Dk Samia amesema serikali itaongeza ushirikishwaji wa vijana katika masuala mbalimbali ili kutoa nafasi kwao kushiriki katika kulijenga taifa akieleza kuwa njia hiyo itasaidia kujenga taifa imara la kesho.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash generating easy and fast method to work part time and earn an extra $15,000 or even more than this online. By working in my spare time I made $17990 in my previous month and I am very happy now because of this job. you can try this now by following
    the details here…… https://Www.Smartpay1.site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button