New York Times yapotosha uhalisia vurugu za uchaguzi

GAZETI la New York Times la Marekani limeandika taarifa inayopotosha ukweli kuhusu vurugu wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, mwaka huu.
Taarifa iliyochapishwa na gazeti hilo haielezi ukweli kuhusu kilichotokea kwa kuwa taarifa hiyo iliandikwa kutoka nje ya nchi. Kwa mujibu wa gazeti la Daily News la Tanzania uandishi wa habari wa namna hiyo ni hatari kwa sababu hauelezi ukweli wa hali ya kisiasa na una lengo la kuridhisha wasomaji badala ya ukweli ulivyo.
“Uhatari wa makala kama haya yaliyoandikwa nje ya nchi ni kwamba haikuitendea haki Tanzania kwani yapo mengi yaliyohitajika kuandikwa lakini yaliachwa na badala yake kujikita kwenye upotoshaji,” ilieleza sehemu ya makala iliyochapishwa katika gazeti la Daily News, Novemba 22 mwaka huu.
Siasa za Tanzania si za upande mmoja Kwenye taarifa ya New York Times ulikosekana muktadha katika eneo la siasa za Tanzania kwa kuwa si za upande mmoja. Gazeti hilo la Marekani lilijikita kwenye taarifa zilizoeleza matukio ya serikali na kutoeleza mengi upinzani.
Vuguvugu la kizazi cha kidijiti lisilo na kiongozi Vuguvugu hilo lilikuwa chanzo kikubwa cha upotoshaji, kuhamasishana mitandaoni na kuzua taharuki kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika. Aidha, kutokana na ombwe la kutopata habari za ukweli kuhusu kilichotokea Tanzania, hadhira ya kimataifa ilijengwa kuamini vurugu za uchaguzi zilisababishwa na ukandamizaji wa serikali.
Madhara yaliyojitokeza Vurugu za wakati na baada ya uchaguzi zilikuwa na madhara mengi yakiwemo vifo vya watu ambavyo ni huzuni kwa familia na Watanzania kwa ujumla huku upinzani ukishangilia kutokana na kile kilichotokea.
Habari ya New York Times inatofautiana na taarifa za ndani ya nchi na ilionesha upotoshaji katika taarifa kuanzia idadi ya vifo bila uthibitisho. SOMA: Hatua ya Rais Samia kusamehe vijana ni funzo la busara
Nani alianzisha vurugu Pamoja na kujulikana wazi kwa walioandaa vurugu hizo gazeti la New York Times halikujihusisha na kuandika ukweli kuhusu vuguvugu la ‘No reforms No election’ lililoratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuvuruga uchaguzi.
“Huu si uvumi. Ilielezwa waziwazi. Imeandikwa mtandaoni. Hurudiwa katika mikutano ya hadhara na kwenye mitandao ya kijamii kuwa watakinukisha lakini gazeti la NYT halikuona hilo,” ilieleza taarifa ya Daily News.
Upotoshaji wa New York Times ulionesha vurugu za uchaguzi zilisababishwa na matendo ya serikali. Pamoja na upotoshaji huo ushahidi unaonesha vurugu zilikuwa zikiandaliwa muda mrefu kabla ya uchaguzi kwa lengo la kuhalalisha vurugu za uchaguzi na kusababisha shutuma za kimataifa.
Sababu halisi za vurugu Ili kuelewa kilichotokea siku ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, swali si, “Nani alipiga risasi kwanza?” badala yake, “Ni nani aliyesababisha hali za vurugu wiki chache kabla ya uchaguzi? Na kwa nini wito wa machafuko uliongezeka siku ya uchaguzi ilipokaribia?” Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Tanzania kwa sasa inakabiliana na vita ya siasa za maneno ikiwemo inayodai kuwa serikali inakandamiza demokrasia.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com