Dk Mwinyi akemea vikao hoteli za kitalii

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameagiza makatibu wakuu wa wizara waache kuidhinisha vikao vifanyike katika hoteli za kitalii.

Dk Mwinyi alitoa agizo hilo wakati akiapisha makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu wa wizara Unguja Novemba 22.

Aliagiza viongozi waongeze kiwango cha makusanyo na wazingatie matumizi bora ya mapato.

“Ukusanyaji umekuwa hafifu lakini matumizi yamekuwa makubwa mno bila sababu za msingi. Unaweza ukakuta mpaka leo kuna watu wanakwenda katika hoteli za kitalii kufanya mikutano, hili jambo sijalielewa,” alisema Dk Mwinyi.

SOMA: Dk Mwinyi: Sitovumilia ugomvi wizarani

Aliongeza: “Wewe kama katibu mkuu mwenye dhamana kweli unaweza ukatoa fedha nyingi watu wakaenda kukaa kwenye hoteli ya kitalii wanafanya kikao cha bodi ya zabuni, haya mambo lazima tuyafikishe mwisho”.

Dk Mwinyi aliagiza viongozi hao waache kufanya kazi wakiwa ofisini kwa kuwa utendaji wa namna hiyo umepitwa na wakati.

“Utenndaji wa sasa unataka tuende tukatatue changamoto za wananchi…kuna matatizo madogo mno lakini yanakaa mwezi mzima, miezi miwili kwa sababu watu wapo ofisini, itoshe sasa. Wananchi wa nchi hii wana matarajio makubwa na sisi,” alisema.

Dk Mwinyi aliagiza viongozi hao watumie vitendea kazi vitano kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo katika kipindi hiki cha pili cha Serikali ya Awamu ya Nane.

Alitaja vitendea kazi hivyo ikiwemo Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2025 hadi 2030.

“Kila mtu akaangalie sekta yake inasemaje katika Ilani, apange mpango kazi wa kuhakikisha kwamba Ilani inatekelezwa kwa asilimia 100,” alisema Dk Mwinyi.

Aliagiza wakaisome hotuba yake wakati akizindua Baraza la 11 la Wawakilishi Zanzibar kwa kuwa kuna maeneo mengi yanayotaka utekelezaji.

Dk Mwinyi alitaja kitendea kazi cha tatu ni ahadi zake wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.

“Ofisi yangu itatoa orodha ya ahadi tulizozitoa kila taasisi na kila wizara ikaangalie maeneo yake kwa madhumuni ya kujipanga kutekeleza katika muda mfupi iwezekanavyo,” alisema.

Dk Mwinyi alisema kitendea kazi cha nne ni Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar na akabainisha kuwa kila mtu anatakiwa aufahamu vizuri na ajipange katika utekelezaji wake.

Alitaja kitendea kazi cha tano ni Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya Mwaka 2025 hadi 2050.

“Tukijipanga vizuri katika utekelezaji wa maeneo haya sina shaka kwamba tutaweza kukidhi matakwa ya wananchi ambayo tuliyasema sana kipindi cha kampeni, Kwangu mimi zile ni ahadi na muungwana akiahidi anatekeleza,” alisema Dk Mwinyi.

Alisema anaamini makatibu wakuu hao wanatambua majukumu yao na kwamba yakiwemo ya kazi za utawala.

“Upande wa pili ni upande wa fedha kwa sababu bila fedha haya yote tunayosema hayatekelezeki. Hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha kama ofisa masuhuli uhakikishe mambo mawili, la kwanza ni kukusanya zaidi na kuzingatia matumizi bora,” alisema Dk Mwinyi.

Alisema watendaji hao lazima wawe na utawala mzuri ili kuepuka makundi.

“Ndani ya wizara zetu mara nyingi unasikia kuna makundi, huyu wake hawa, huyu wake wale, tukienda hivyo hatuwezi kutekeleza kazi zetu. Niwatake ninyi kama ni watawala mhakikishe kwamba mnaondoa hayo makundi, watu wote wanakuwa lao moja mnafanya kazi ya wananchi waliotukabidhi,” alisema Dk Mwinyi.

Dk Mwinyi ameagiza waondoe makundi katika maeneo yao watu wote wawe kitu kimoja na kufanya kazi ya wananchi waliyowakabidhi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button