Niffer akwama, wenzake 20 wafutiwa mashitaka

DAR ES SALAAM; MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) amesema hana nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa 20 kati ya 22 walioko katika kesi ya uhaini inayomkabili  mfanyabiashara Jennifer Jovin(26) na wenzake 21.

Hayo yameelezwa Wakili wa Serikali, Titus Aaron leo Novemba 25,2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam , mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya kesi hiyo ilipopelekwa kwa ajili ya uamuzi wa hoja zilizowasilishwa  na jopo la upande wa mawakili wa utetezi ukiongizwa na Wakili Peter Kibatala.

Awali Wakili Aaron alidai shauri hilo lilipelekwa kwa ajili ya uamuzi, lakini chini ya kifungu cha 92(2) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA)sura ya 20 urekebu wa 2023, DPP amesema hana nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa 20 kati ya 22 waliopo katika kesi hiyo.

Pia alidai DPP anaendelea kuwashitaki washitakiwa wawili katika shauri hilo ambaye Niffer na mshitakiwa namba 17 ambaye ni Mika Chavala(32).

Baada ya kuelezwa hayo Hakimu Lyamuya alisema kama ilivyoelezwa kuwa DPP hana nia ya kuendelea kuwashitaki mshitakiwa wa pili hadi 16 na wa 18 hadi 22. Lakini washitakiwa wawili ambao ni Niffer na Chavala  alisema watarudi rumande kwa kuwa DPP bado ana nia ya kuendelea kuwashitaki.

Kuhusu uamuzi uliotakiwa kutolewa leo juu ya pingamizi zilizowasilishwa na Wakili Kibatala na wenzake kuhusu shitaka la kwanza kuondolewa, Hakimu Lyamuya alisema hana mamlaka ya shauri hilo kwani hiyo ni mahakama kabidhi tu. Kesi imeahirishwa hadi Desemba 3, 2025 kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande.

Washitakiwa walioachiwa katika kesi hiyo ni  kesi hiyo ni Mwalimu, Lucianus Luchius (28), Paul Malima (28), Augustino Mulwale (30), Mohamed Kondo (30), John Mmena (26), Paul Shirima (23), Ramadhani Ramadhani (21), Levi Mkute (40), Esau Ernest Maarufu ‘Duduye’ (21), Leonard Mkonyi.

Wengine ni Fadhili Nyombi, Hamisi Hamisi, Abeid Kivuyo (24), Nicholous Shiduo (27),Abati Mwadini (27), Fatuma Mzengo (30), Dewji Ramji (19), Ruthmelda Silaa (21), Hilda Ngulu(22) na Yusuph Hussein(22)

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka ilidaiwa kuwa katika tarehe tofauti kati Aprili Mosi,2025 na Oktoba 29, 2025, katika maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya ya Ubungo, Mkoa wa Dar es Salaam,walikula njama na kupanga kwa siri kufanya kosa la uhaini.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button