Tanzania yalionya bunge la Ulaya kuingilia siasa zake

TANZANIA: TAIFA la Tanzania limekosoa vikali kile inachokiita ongezeko la uingiliaji wa kisiasa kutoka mataifa ya kigeni, baada ya Bunge la Ulaya kupanga kufanya kikao kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu baada ya uchaguzi bila kushauriana na serikali yenyewe.
Hatua hiyo imeibua mvutano ambao wachambuzi wanasema ni shinikizo la nje.
Katika barua ya kidiplomasia ya Novemba 25, 2025, Ubalozi wa Tanzania mjini Brussels ulieleza wasiwasi mkubwa juu ya mpango wa Bunge la Ulaya kujadili mauaji baada ya uchaguzi na hali inayodorora ya haki za binadamu ikiwemo sakata la mwanasiasa wa upinzani Tundu Lissu.
Serikali ilisema hatua hiyo imechukuliwa bila kuiwezesha Serikali kutoa ufafanuzi wake na kuweka ukweli wazi jambo ambalo, kwa mujibu wake, linapuuza misingi ya haki ya kusikilizwa na kanuni za mazungumzo zilizowekwa katika Mkataba wa Samoa unaosimamia mahusiano ya EU na OACPS.
Kwa mujibu wa barua hiyo, vifungu 2(3), 5 na 87(1) vya mkataba huo vinatilia mkazo mazungumzo, mashauriano na kuheshimiana kama msingi wa kutafuta ufumbuzi wa migogoro. Tanzania ilionya kwamba kuendelea na kikao kwa kutegemea taarifa za upande mmoja kunaweza kudhoofisha uadilifu wa ushirikiano uliojengwa kwa miaka mingi.
Upinzani huo wa Tanzania unakuja wakati maofisa wa serikali na wachambuzi wa ndani wakionya kuhusu kile wanachoona kama kampeni iliyoratibiwa na wahusika wa nje serikali, wanadiplomasia, mashirika yasiyo ya kiserikali na vyombo vya habari vya kimataifa wanaojaribu kushawishi siasa za ndani kwa kisingizio cha haki za binadamu na utawala bora.
Katika wiki za hivi karibuni, Media Wire Express imeripoti matamko ya kimataifa, shinikizo la kidiplomasia na wimbi la waandishi wa habari kutoka nje wanaoendeleza simulizi ambayo, kwa mujibu wa maofisa waandamizi, hayalingani na hali halisi nchini.
Vyanzo vya serikali vinasema vurugu zilizotokea majuzi, ikiwemo matukio ya ukatili, zilichochewa na makundi yanayopokea ufadhili kutoka nje. “Kuna mtindo unaojitokeza,” alisema afisa mwandamizi kwa sharti la kutotajwa.
“Pale mataifa huru yanapochukua maamuzi ya kisiasa au kiuchumi yasiyolingana na maslahi ya mataifa yenye nguvu, zana za shinikizo huanza kuibuka matamko, vikwazo, kusimamishwa kwa misaada, na taarifa zilizopangwa kwenye vyombo vya habari. Tumeliona hili mara nyingi barani Afrika.”
Wakosoaji wanataja kile wanachoona kama upendeleo katika utetezi unaofanywa na mataifa ya Magharibi na taasisi zake. Wakati Bunge la Ulaya likiandaa kuichunguza Tanzania, kumekuwa na ukimya kuhusu vifo vya raia Sudan au mashambulizi yanayoendelea Gaza.
“Kama kiwango kile kile kingetumika duniani kote, serikali nyingi zingekuwa zinafikishwa kwenye vikao kila wakati,” amesema mchambuzi wa kisiasa wa ukanda huo. “Kimya kwenye baadhi ya migogoro na kelele kwenye mingine si bahati mbaya. Ni maslahi ya kijiografia, si msimamo wa kibinadamu.”
Barua ya Ubalozi pia ilibainisha kwamba Tanzania tayari imeunda Tume Huru ya Uchunguzi kuchunguza matukio yaliyotokea. Maofisa wanasema shinikizo la nje linaweza kuathiri kazi ya taasisi za ndani hata kabla hazijamaliza uchunguzi.
Wanadiplomasia mjini Brussels waliiambia Media Wire Express kwamba Tanzania imeomba kikao hicho cha bunge kuahirishwa ili kuiwezesha serikali kutoa maoni yake. Iwapo jambo hilo halitowezekana, imeomba iruhusiwe kuzungumza wakati wa kikao. Kufikia Jumatano, Bunge la Ulaya halikuwa limetoa majibu ya wazi.
Mvutano huu unaongeza moto kwenye mjadala mpana barani Afrika kuhusu uingiliaji wa kigeni na mamlaka ya nchi, huku baadhi ya viongozi wakionya kwamba mataifa makubwa yanazidi kutumia hoja za haki za binadamu, mashirika ya kiraia na taasisi za kimataifa kuathiri matokeo ya kisiasa katika mataifa yanayoendelea.
Kwa Tanzania, mvutano huu mpya unathibitisha wasiwasi wa muda mrefu kwamba washirika wa kimataifa wanatoa hukumu haraka bila kuingia kwenye mazungumzo. Bunge la Ulaya litasitisha hatua yake au litaendelea bila kumsikiliza Dar es Salaam huenda ndilo litakaloamua kwa kiasi kikubwa mustakabali wa mahusiano ya pande hizo katika miezi ijayo.




Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com