Watanzania wanufaika ajira viwanda vya wazawa

MOROGORO: WAWEKEZAJI wazawa wa viwanda vinavyotumia malighafi zitokanazo na mazao ya kilimo wameendelea kufungua milango ya ajira kwa Watanzania na upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa wakulima nchini.

Hayo yamebainika katika Maadhimisho ya Maonesho ya Biashara ya Mkoa wa Morogoro yaliyofanyikauwanja wa Jamhuri mkoani hapa.

Msaidizi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mambo Coffee, Hadija Kajia amesema kiwanda cha Mambo Cofee ambacho makao yake makuu ni Manispaa ya Morogoro, kinamilikiwa na Mtanzania na kimetoa ajira za kudumu kwa watu 34 na vibarua 20.

Kajia  amesema kiwanda hicho kipo katika nyanja ya kijamii na kukuza kipato cha mkulima mdogo kwa kununua  zao la kahawa kuchakata na lengo ni kuendelea kununua zao hilo  kutoka akwa wakulima wengi zaidi hapa nchini.

“Kwa upande wa wakulima tunafanya kazi na Amcos kwa maana vyama vya ushirika na vinakitambua kiwanda cha Mambo Coffe kurtokana na uhakika wa soko,” amesema Kajia .

Anasema kwa mkoa wa Morogoro kiwanda kinafanya kazi na wakulima wachache ambao wanakiletea kiwanda kahawa.

“Kwa sasa tunatarajia kwenda kuendesha  mafunzo kwa wakulima kna tupo kwenye mchakato mwakani Februari  2026, mafunzo hayo yatatolewa kupitia mtaalamu wetu wa kilimo hai,” alisema Kajia.

Kajia anasema baada ya kupatiwa mafunzo hayo wakulima watakuwa wamepata elimu, ujuzi na uwezo wa kuongeza uzaliahaji wa zao la kahawa, jambo ambalo ni faida kwao na kwa kiwanda.

“ Sisi Kiwanda tutakuwa na uhakika wa kupata malighafi ya zao hilo na wao wakulima kuwa na uhakika wa kupata masoko,“ amesisitiza Kajia.

Amesema kuwa wakulima wa Tarafa ya Mgeta, Wilaya ya Mvomero mkoani humo wanaendelea kunufaika na  uwepo wa kiwanda hicho ambapo wameweza  kuuza kontena moja .

Kajia amesema kutokana na shughuli za ununuzi wa zao la kahawa  na kuuza nje ya nchi, Kiwanda kinachangia kukuza pato la kiuchumi la Taifa ikiwa na kulipoa ushuru wa masuala mbalimbali kwenye ununuzi , uuzaji na usafirishaji wa kahawa .

“Nawashauri wananachi kupenda kunywa kahawa kwani licha ya kuburidisha, bali  inachangia kujenga afya hasa kwa watu wenye shinikizo  la chini la damu ,unashauriwa na madaktari kunywa kahawa ili kuipandisha kufikia kiwango kinachohitajika mwilini,”amesema Kajia.

Naye Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo anayeshughulikia uwekezaji, viwanda na biashara, Beatrice Njawa,amesema kupitia maonesho hayo, serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya kuendeleza sekta binafsi, wajasiriamali na wafanyabiashara kwa lengo la kukuza mitaji na kuongeza mchango wao katika uchumi wa taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), mkoa huo  Muadhini Mnyanza, amesema waoneshaji 117 waliweza kushiriki katika monesho ya  biashara ya mkoa .

Mnyanza amesema  kuwa mafanikio ya maonesho hayo ni ishara ya mwitikio mzuri kutoka kwa wadau wa biashara na uwekezaji ,na walipokea  maoni mbalimbali kutoka kwa washiriki kwa ajili ya kuyafanyia kazi ili kuyaboresha zaidi katika miaka ijayo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button