Mwigulu afunga semina ya Mawaziri

WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba leo Desemba 04, 2025 amefunga semina elekezi kwa Mawaziri na Naibu Mawaziri iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

SOMA: DK Nchimbi aapishwa kuwa Makamu wa Rais

Semina hiyo ambayo ilifunguliwa na Makamu wa Rais, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi ilikuwa na lengo la kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu majukumu, taratibu, maadili na matarajio ya Serikali kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika semina iliyoandaliwa kwa ajili ya Baraza la Mawaziri, Dk Mwigulu amesema kuwa maarifa waliyoyapata yatasaidia kuwaongoza katika kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, Rasilimali za Umma, Dira 2050, Mipango ya Maendeleo na kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button