Abuni mabaki makaa ya mawe kuwa mkaa

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM), Anna Emanuely amebuni njia ya kubadili vumbi au mabaki ya makaa ya mawe yatumike kama mkaa.

Hayo yamebainika wakati Asha alipozungumza na HabariLeo katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ( DITF) nayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba.

Kwa maelezo ya mwanafunzi huyo hiyo ni njia mbadala ya kutatua changamoto ya uharibifu wa mazingira ya ukataji miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa.

Amesema Vumbi au mabaki hayo yanayotokana na uchimbaji wa makaa ya mawe katika maeneo ya migodi yamekuwa chanzo kikubwa na uharibifu wa mazingira unaosababisha mabadiliko ya tabia nchi.

“li kukabilianana na changamoto ya uharibifu huo wa mazingira ni kubadilisha vumbi hilo litumike kama mbadala wa mkaa na kuni, njia ambayo itasaidia kuzuia uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti ovyo,” amesema.

Mkaa huo wa vumbi hilo una ubora wa kiwango cha juu kwa kuwa kipande kimoja kina uwezo wa kutumika kupikia kwa saa 12..

“Sasa unakuta vumbi linachukua eneo kubwa na linaonekana kama uchafu, sisi tunakusanya lile vumbi la makaa ya mawe na kuchanganya na udongo, pumba na chokaa kisha tunaweka maji kwa ajili ya kutengeneza donge la mkaa,” amesema.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Masoko MUCE, Dk Ponsiano Kanijo anasema kama taasisi nyingine za elimu ya juu chuo hicho kimejikita kwenye kufundisha, kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalam kwa jamii.

“Katika kuunga mkono jitihada za Serikali kwenye sayansi na masuala ya utafiti na ubunifu, Chuo hutenga fedha kwenye bajeti yake kila mwaka.

“Kwa mwaka wa fedha uliopita, yaani 2022/2023 na mwaka huu wa fedha 2023/2024, Chuo kimetenga fedha kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 350,” amesema.

Anasema kuanzia mwaka wa fedha huu wa 2023/2024 kiasi cha fedha hizo kitaanza kutumika kuwasaidia watafiti kuandika tafiti kubwa zitakazokisaidia mabadiliko makubwa kwenye jamii.

Anaeleza kuwa Chuo, kupitia Kiota kitahakikisha Anna anasaidiwa kuendeleza utafiti huo ili aanze kuzalisha mkaa huu.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button