ACT: Kipaumbele ni mageuzi ya kisiasa

DAR ES SALAAM: KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amesema suala la kushiriki au kutoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2025, sio kipaumbele cha chama hicho kwa sasa, kwani uamuzi wa mwisho kuhusu hilo utafanywa na Kamati ya Uongozi Taifa.
Kiongozi huyo ameeleza kuwa mkazo wa ACT Wazalendo kwa sasa ni kupigania mageuzi ya kisiasa nchini.

Dorothy amezungumza hayo leo Machi 27 alipofanya mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Tanzania, Theresa Zitting, katika kikao kilichohudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu, Ester Thomas, Katibu wa Mambo ya Nje, Mwanaisha Mndeme, na Katibu wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa Umma, Shangwe Ayo.
Dorothy ataendelea na ziara kwenye taasisi mbalimbali za ndani na kimataifa, kuelezea msimamo na mwelekeo wa ACT Wazalendo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.




