ACT Wazalendo kusherehekea utumishi wa Juma Duni

KATIKA kutekeleza agizo la Kikao cha Halmashari Kuu ya Chama Cha ACT Wazalendo  kilichoketi cha Agosti 25 2024, chama hicho kimeandaa shughuli ya kusheherekea maisha na utumishi wa mwenyekiti  mstaafu wa chama hicho, Juma Duni Haji.

Tukio hili linatarajiwa kufanyika Septemba 4, 2024 katika Ukumbi wa Majid Hall, Kiembe Samaki kuanzia saa 3.00 asubuhi.

SOMA: Wazalendo wateua manaibu katibu wakuu Bara, Zanzibar

Tukio hilo litalowaleta pamoja wanachama na viongozi wa ngazi mbalimbali kusheherekea maisha na utumishi wa Juma Duni Haji ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya ACT Wazalendo ya kuwaenzi viongozi wastaafu iliyotungwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho Machi 2024.

Habari Zifananazo

Back to top button