Ado amtumia salamu Shigongo

KATIBU Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema ameduwazwa na jinsi Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo alivyoshindwa kutatua changamoto za barabara, vivuko, maji na pembejeo kwenye jimbo lake la Buchosa na kumtaka ajiandae kung’oka 2025.

“Shigongo anajipambanua kwa umashuhuri, ujenzi wa hoja na mtandao lakini niseme kwa niliyoyaona Buchosa, amewatelekeza wananchi wake, ajiandae kuondoka 2025 kama hatashughulikia changamoto za barabara, maji, vivuko na mbolea ya ruzuku,” amesema Ado Shaibu.

Advertisement