MAREKANI : UMOJA wa Mataifa umeonya kuwa uamuzi wa Taliban wa kuwazuia wanawake kusomea utabibu kutaharibu hali zaidi Afghansitan inayokabiliwa na changamoto za kibinadamu.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , Tom Hetcher amesema katika kikao cha baraza la usalama la umoja wa mataifa wamesema uamuzi huo wa kusitisha mafunzo kwa matabibu wa kike nchini Afghanistan utachangia kudhorotesha utoaji wa huduma za afya kwa wanawake na wasichana nchini humo.
Mapema mwezi huu, utawala wa Taliban uliamuru vyuo vya umma na binafsi vya kutoa mafunzo ya utabibu visitishe mara moja kuandikisha wanafunzi wanawake pamoja na kuwazuia kumaliza mitihani yao ya mwisho wa muhula. SOMA : Madaktari 42 Tanzania waimarishwa utoaji huduma
Hata hivyo amri hiyo ya ghafla ilitoa muda wa siku kumi kwa vyuo hivyo kuwaruhusu wanafunzi wa kike kufanya mitihani ya muhula.
Sekta ya afya ndiyo pekee iliyokuwa imebaki kwa wanawake wa Afghanistan kupata elimu ya juu kufuatia kupigwa marufuku kwa elimu ya juu ya wanawake na serikali hapo nyuma.
Hetcher amesema hatua hiyo itaathiri zaidi ya wakunga 36,000 pamoja na wauguzi 2,800 waliokuwa kwenye sekta ya ajira katika miaka michache ijayo, na viwango vya vifo vya watoto huenda vikaongezeka, vifo vya wajawazito pamoja na akina mama nchini humo.