Afisa mkuu wa mapato Burundi afutwa kazi

BURUNDI : MKURUGENZI MKUU wa makusanyo ya mapato ya serikali nchini Burundi, Obr Manirakiza Jean Claude amefutwa kazi na Rais Evariste Ndayishimiye na kumteuwa Emmanuel Mbonihankuye kuchukua wadhifa huo.

Jean Claude Manirakiza  anatuhumiwa kuweka wazi upungufu wa kiwango cha mapato kinachokusanywa na taasisi yake katika kipindi cha miezi minne iliyopita.

Afisa huyo alinukuliwa wakati wa maadhimisho ya siku ya mlipa kodi Desemba 3.  SOMA: Burundi kuunganishwa na Mkongo wa Taifa

Advertisement

Hivi karibuni Mkuu wa Shirika la kupambana na rushwa nchini humo  Gabriel Rufyiri alikiri kuwa taasisi hiyo ya ukusanyaji wa mapato haiwezi kufanikisha majukumu yake itasalia kuwa chini ya mamlaka ya rais.

Burundi inakabiliwa na changamoto za kiuchumi ambapo mwezi uliopita sarafu ya faranga imekuwa ikishuka thamani na kusababisha mfumuko wa bei za bidhaa.