Afrika iwekeze tafiti za kilimo kuwawezesha vijana – Kikwete

ARUSHA: NCHI za Afrika zinahitaji kuwekeza zaidi katika utafiti na kilimo ili kuwawezesha vijana kupata mwelekeo wa maendeleo kwa ajili ya kupunguza na kuondoa umaskini katika bara hilo.

Pia matumizi ya takwimu sahihi katika kutunga sera za kupambana umaskini ni jambo la kuweka kipaumbele.

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa kujadili masuala ya umaskini, ulioandaliwa na Shirika la Usimamizi wa Sera ya Oxford Tanzania (OPM) kwa kushurikiana na mashirika mengine.

JK: Rais wa Namibia mfano wa kuigwa Afrika

Amesema mapambano dhidi ya umaskini yanahitaji mshikamano wa kitaifa na kimataifa, kwani haupaswi kuendelea kuishi katika dunia yenye utajiri mwingi, huku mamilioni wakikosa mahitaji ya msingi kama chakula, elimu na huduma za afya.

“Miaka mitano kuelekea mwisho wa mwaka 2030 katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa bado tupo nyuma lakini hii ni kwa sababu ya shida iliyopatikana katika miaka mitano iliyopita, pamoja na janga la ulimwengu la Covid-19, vita vya jiografia na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa,” amesema.

Amesema chini ya kipimo kipya, watu wanaodhaniwa kuwa wanaishi katika umaskini uliokithiri sasa wanaelezewa kuwa wale wanaoishi chini ya USD 3.0 kwa siku na kuongeza kuwa kila Rais kwa awamu yake kwa upande wa Tanzania alijitahidi kuhakikisha anatekeleza Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050 katika kupunguza umaskini na kuingia katika nchi za uchumi wa kati”

Naye, Mkurugenzi wa Nchi wa Usimamizi wa Sera ya Oxford (OPM) nchini Tanzania, Dk,Charles Sokile alisema kwamba hapo zamani watu wanaoishi chini ya USD 1.25 walizingatiwa kuwa chini ya umaskini mkubwa na kusisitiza kilimo pamoja na utafiti utawezesha kujua viwango via umaskini na mbinu za kujikwamua kiuchumi

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button