Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Sarah Mwaipopo amefungua mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuhusu sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Cha Uongozi wa Mwalimu Nyerere Kibaha mkoani Pwani.