Agha Khan, Muhimbili wafanya operesheni 23 kuboresha maumbile

HOSPITALI ya Aga Khan, kwa kushirikiana na shirika la Kimataifa la Reconstruction Woman International (RWI) na Hospital ya Taifa ya Muhimbili wamefanya kwa mafanikio operesheni 23 za kubadili na kuboresha maumbile ikiwemo matiti kwa wanawake na wasichana nchi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Aga Khan, Dkt Aidan Njau, amesema upasuaji huo ni bure kwa kubadili na kuboresha maumbile unafanywa Mara moja kila mwaka walianza tangu 2016 hospital hapo kwa kuzingatia vigezo.

Amesema upasuaji huo unaongozwa na timu ya madaktari bingwa wa upasuaji wa kubadili na kuboresha maumbire kutoka Marekani, Canada na Ulaya wanaoshirikiana kwa karibu na wataalamu wazawa wa Tanzania ili kuwajengea uwezo na kufanya upasuaji.

“Kusudi la mpango wa matibabu haya ni kurejesha utendaji kazi ufanisi wa viongo vilivyoathirika na majanga ya ajali ya kwenye mwili wa mwanamke na msichana pamoja na wenye maziwa makubwa yanayowanyima kujiamini na kuwarejeshea furaha yao.”amesema Njau

Habari Zifananazo

Back to top button