WATU 13 wamepoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya Fuso waliyokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kutumbukia mtoni majira ya saa 2: 30 usiku wa kuamkia leo.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Ndile amesema gari hiyo ilikuwa imebeba wafanyabiashara waliokuwa wakitoka mnadani katika kijiji cha Ndongosi na walikuwa wakielekea kijiji jirani cha Namatuhi wilayani humo.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Songea na tayari ndugu wameitambua miili hiyo. DC Ndile amesema majeruhi wanaendelea na matibabu katika kituo cha Afya cha Namanditi.