Akimbia Kilometa 90 kumthibitishia mchumba waoane

Mwanaume mmoja huko Afrika Kusini amejipatia umaarufu katika mitandao ya kijamii, baada ya kukimbia umbali wa Kilometa 90 kumthibitishia mpenzi wake Prudence kuwa amefika mwisho wa kutafuta na kwamba anataka wawe mume na mke.

Joseph Kagiso Ndlovu mzee wa miaka 57, amesema amekimbia umbali huo, ili ampose mwanamke aliyetajwa kwa jina la Prudence.

Joseph alipigwa picha akiwa ameshika bango la kumtaka mwanamke huyo amuoe, alipokuwa akikaribia kumaliza mbio za Comrades Marathon siku ya Jumapili.

“Prudence utanioa? Nimekimbia 90 kilometa kwa ajili yako,” aliandika katika bango.

Vyombo vya habari vya ndani na watumiaji wa mtandaoni wamekuwa wakihoji umbali, ambao mwanaume anapaswa kwenda kumtongoza mpenzi wake

Habari Zifananazo

Back to top button