Algeria, Nigeria, Niger kusafirisha gesi asilia Ulaya

ALGERIA : MAAFISA  kutoka nchi za Algeria, Nigeria na Niger wamesaini  mikataba mipya inayolenga kuharakisha uendelezaji wa bomba kubwa la gesi asilia linaloelekea Ulaya.

Bomba hili, ambalo lilitangazwa mwaka 2009, litatumika kusafirisha mabilioni ya mita za ujazo za gesi kutoka Nigeria kupitia Niger hadi Algeria.

Gesi hiyo itasafirishwa kupitia bomba la chini ya bahari kuelekea Italia, au kupakiwa kwenye meli za gesi asilia zilizowekwa kimiminika na kusafirishwa nje ya nchi.

Advertisement

Nchi hizo tatu zimesaini mikataba inayohusu ripoti ya upembuzi yakinifu na masuala mengine, pamoja na makubaliano ya kimkakati kati ya makampuni ya nishati ya serikali.

Mradi huu unapata msukumo mkubwa kutokana na ongezeko la mahitaji ya gesi duniani na kupanda kwa bei, hasa baada ya vita vya Urusi na Ukraine vilivyovuruga soko la nishati.

SOMA: ‘Tunataka gesi asilia ibadili maisha ya watu’

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *