MGONJWA aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) ambaye video yake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha akibusu midomo na ndimi na mpenzi wake wodini ameomba radhi kwa kitendo hicho na kuahidi hatorudia tena.
Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Moi, Patrick Mvungi inasema kuwa kitendo kilichofanywa na mgonjwa huyo na mpenzi wake nii kinyume cha maadili .
Mvungi amesema kitendo hicho kimefanyika katika Wodi 3A siku ya Jumapili mchana Julai 9, 2023.
Amesema katika uchunguzi wa awali mgonjwa amekiri kufanya tendo la busu la midomo na ndimi na mpenzi wake katika mazingira ya kuumwa ndani ya Hospitali kitu ambacho ni kinyume na maadili ya Tanzania.
“Menejimenti imebaini kwamba mpenzi wa mgonjwa huyo si mtumishi wa Moi.”Amesema
Amesema, tukio hilo liligunduliwa na muunguzi aliyekuwepo wodini ambapo alichukua hatua ya kuzuia wahusika kuendelea na kitendo hicho na menejimenti inaendelea kuchukua hatua zaidi kwa wahusika.
“Uchunguzi umebaini pia wakati vitendo vinaendelea kuna mgonjwa Jirani (jina limehifadhiwa) ambaye alisharekodi, Moi inalaani kitendo hichocha uvunjivu wa maadili kilichofanywa na mgonjwa pamoja na mpenzi wake.
“Vilevile Menejimenti inaalaani na kukemea kitendo cha kurekodiwa video wodini na kutuma kwenye mitandao ya kijamii kilichofanywa na mgonjwa jirani.”Amesema
“Matukio haya yote ni kinyume na mwongozo wa Wizara ya Afya unao zuia kufnaya matendo ya uvunjifu wa maadili kwa mgonjwa na kurekodi video wodini.
Menejimenti inaendelea kuchunguza zaidi tukio hili ili kujiridhisha kuwa hapakuwa na uzembe katika kusimamia usalama wa wagonjwa wakati ndugu wanawatembelea wagonjwa wodini.
Amesema Moi inaendele kuwakumbusha wagonjwa pamoja na ndugu wa wagonjwa kuheshimu miongozo ya Wizara ya Afya kwa kutofanya vitendo vyenye uvunjifu wa maadili au kupiga picha video katika maeneo ya kutolea huduma za afya
Comments are closed.