KENNEDY NYANGIGE mwenye umri wa miaka 20, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya Bugando (Cuhas), anashikiliwa na polisi mkoani Mwanza akidaiwa kutoa taarifa za uongo kuwa ametekwa na watu wasiofahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroard Mutafungwa amesema wa kusoma huyo alitoa taarifa za uongo kwa familia yake kwamba ametekwa na watu wasiofahamika na yupo sehemu isiyojulikana, hivyo kwa kutumia simu yake watekaji walitaka watumiwe Sh milioni 3.
5, ili wamuachie vinginevyo angeuawa.
Kamanda amesema baada ya taarifa hiyo kuripotiwa polisi, walianza uchunguzi wa kina na kumkuta kijana huyo katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Fm Katapila iliyopo Kata ya Igogo, wilayani Nyamagana, akiwa amejifungia ndani chumba namba 103, huku akiendelea kunywa pombe.