Aliyekuwa mke wa Dk mwaka awatia moyo wanawake

ALIYEKUWA mke wa Dk Mwaka, Queen Oscar amewataka wanawake kutoogopa kuanza maisha upya pindi wanapokutana na changamoto ya manyanyaso au vitisho kutoka kwa mumewe kwakuwa mwanamke sio kiumbe dhaifu ila amekuwa na utii kwa mumewe.

Akizungumza jana mkoani Dar es Salaam wakati akipokea ubalozi wa kampuni ya magari ya Bm Car Dealers, Queen alisema aliamua kuachana na kila kitu cha mumewe ikiwemo nyumba na mali kwakuwa anaamini anaweza kusimama mwenyewe.

Alisema aliachana kufanya kazi kwa zaidi ya miaka kumi ili kulea familia, lakini kutokana na kuanza maisha yake na watoto wake ameamua kurudi tena kazini ili kusimama mwenyewe.Queen alisema mwanzo alikuwa akilalamika kutishiwa maisha na kuishi kwa wasi wasi muda wote, lakini tayari taarifa ameshaifikisha polisi, hivyo haoni sababu ya kuendelea kuishi kwa wasi wasi na kuamua kuishi maisha yake mwenyewe bila ya kujificha.

“Unapokuwa mama unatulia na kuangalia mwanamme anafanya nini, kuna wakati unasimama kwa miguu yako na kuendesha familia yako, mimi ni mwanamke lakini pia ni mama nahitaji kuleta mchango wangu kwa jamii,” alisema.

Alisema kwa sasa ni mfanyakazi na balozi wa kampuni ya kununua magari kwa njia kulipia kidogo kidogo kupitia kampuni ya Bm Car Dealer, ambapo anatarajia kuanzisha kampeni ya Gari ya mama yangu.

Kampeni hiyo inayotarajia kufanyika Mei 14 Siku ya mama duniani lengo ni kushawishi watu kununulia magari mama zao badala ya kumnunulia mke au mume kama ilivyozoeleka.Alimalizia kwa kusema kwa sasa hatopigania tena taraka, kwakuwa anaamini ni jambo ambalo litamfuata.

Habari Zifananazo

Back to top button