Antony Joshua kutwangana na Dubois au Fury

Bondia Anthony Joshua

BONDIA wa uzito wa juu Anthony Joshua atazichapa na ama Daniel Dubois au Tyson Fury katika pambano lijalo, amesema promota wake, Eddie Hearn.

Joshua mwenye umri wa miaka 35 alipoteza pambano lake la nne aliposhindwa kutamba mbele ya bingwa wa dunia anayetembuliwa na Shirikisho la Ndondi la Kimataifa(IBF) Septemba mwaka huu katika uwanja wa Wembley, London.

SOMA: Dubois amtisha Joshua pambano la IBF

Advertisement

Fury ambaye amehusishwa kwa muda mrefu kuzichapa na Joshua, atapanda ulingoni Desemba 21 mwaka huu kupambana na Oleksandr Usyk wa Ukraine baada ya kupoteza kwa Myukraine huyo Mei mwaka huu.

“Tunakwenda kupigana na Dubois au Fury. Ndio hivyo. Hatuna nia nyingine wala pambano la maandalizi,” amesema Hearn.

Dubois mwenye umri wa miaka 27, alimpeleka mara kadhaa sakafuni Joshua mbele ya idadi iliyoweka rekodi ya wingi wa mashabiki 96,000 kabla ya pambano kusimamishwa katika raundi ya tano.