Dubois amtisha Joshua pambano la IBF

BONDIA Daniel Dubois ameapa kumtwanga makonde ya kutosha bondia mwingereza mwenzake Anthony Joshua kwenye pambano la uzito wa juuu litakalofanyika Septemba 21 uwanja wa Wembley, London.

Siku mbili baada ya Joshua kutangaza kwamba anakusudia kufia ulingoni ili kuwa bingwa mara tatu wa dunia wa uzito huo, mfalme wa Shirikisho la Kimataifa la Ndoni (IBF) Dubois amsisitiza kuwa mpinzani wake huyo mwenye uzoefu atapata kichapo cha hatari.

SOMA: Usyk bingwa asiyeshindika, amduwaza Fury

Advertisement

“Nahitaji kumrudisha mahali pa giza na kumfanya asiwe na furaha, kumfanya apasuke ndani ya ulingo. Hilo ndilo ninapanga kufanya,” amesema Dubois.

IBF inasimamia mashirikisho rasmi ya ndondi 198 duniani.