Apongezwa kuvuna ‘Cha Arusha’

MLIMWA, Dodoma: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya namna inavyodhibiti biashara ya dawa za kulevya nchini.

Akiwasilisha pongezi hizo kwa Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo (DCEA), Aretas Lyimo wakati wa hafla ya Futari aliyoiandaa kwaajili ya watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake leo, eneo la Mlimwa jijini Dodoma, Majaliwa amesema ukamataji uliofanyika kipindi hiki haujawahi kutokea kabla.

“Ameenda shambani mpaka kule Arusha, amevuna ‘Cha Arusha’ chote,” amesema kiongozi huyo.

Amesema, DCEA amefanya kazi nzuri na hilo linathibitika kwa namna alivyoboresha sekta yake. Hivi sasa taasisi yake haiishii tu Makao Makuu ya Nchi ila ameshusha hadi kwenye kanda.

“Tayari wakurugenzi wameshaenda kwenye maeneo hayo ambao watakamata wazalishaji, wasafirishaji, wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za kulevya,” amesema Majaliwa.

Habari Zifananazo

Back to top button