VETA, vituo vya malezi kushirikiana kutoa ujuzi

DODOMA: MKURUGENZI wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Anthony Kasore amesema mamlaka itaendelea kushirikiana na vituo vya malezi ya watoto ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi utakaowawezesha kujitegemea na kuchangia maendeleo ya taifa.

Akizungumza wakati wa kuwafuturisha watoto kutoka kwenye vituo viwili vya malezi ya watoto vya jijini Dodoma, Kasore alisema ushirikiano huo utahusisha maeneo mbalimbali ikiwamo malezi pamoja na utoaji wa mafunzo ya stadi za kazi.

“Na sisi kama mamlaka tunasema kuwa tutazidi kushirikiana na wenzetu kutoka kwenye nyumba hizi za malezi ya watoto ili kuhakikisha vijana hawa wanapata ujuzi utakaowasaidia katika maisha yao,” alisema.
Kasore alisema kuwa jukumu la VETA ni kuhakikisha vijana wanapatiwa ujuzi unaowawezesha kuwa raia wema, wanaojitambua, wanaolipenda taifa lao na wenye uwezo wa kujipatia kipato na kuchangia pato la taifa.

“Tunataka kuwaona vijana hawa wanakuwa raia wanaoweza kujitegemea na pia kuchangia pato la taifa kupitia ujuzi watakaoupata.”

Kasore alifafanua kuwa VETA ina wajibu wa kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali ya Watanzania, hususan vijana, ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha.

Alisema lengo la kukutana na watoto hao, mbali na kufuturu pamoja, pia ni katika kuwajengea uelewa kwamba maisha yana changamoto mbalimbali zinazohitaji ujuzi ili kuzishinda.

SOMA: Biteko atia neno mjadala wa VETA

“Tunataka vijana watambue kuwa katika kuishi, kuna mengi tunakutana nayo, hivyo ni muhimu kupata ujuzi utakaotusaidia katika nyanja mbalimbali za maisha,” alisema.

Aidha, Kasore alibainisha kuwa moja ya majukumu makuu ya VETA ni kusaidia kutafsiri ndoto za vijana kwa kuwapatia ujuzi unaowawezesha kuzitimiza.

“Tunapokaa na nyie tunaamini tunaweka msingi imara utakaowasaidia kuelewa kuwa pamoja na elimu, ni muhimu pia kupata ujuzi utakaowaongoza katika maisha ya baadaye.”

Kwa upande wa Afisa Tarafa wa Dodoma Mjini, Zainabu Mabuya aliipongeza VETA kwa kuwakumbuka watoto wenye uhitaji na kutoa wito kwa taasisi na jamii kwa ujumla kuendelea kuwasidia wahitaji.
Pia alipongeza juhudi za VETA za kuendelea kutoa mafunzo kwa makundi maalumua ya wanawake na vijana wa bodaboda ambao sasa wamekuwa wakiendesha maisha na kuchangia uchumi wa nchi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button