Apongezwa kwa kupanda mlima Kilimanjaro mara 50

SERIKALI imempongeza balozi nguli wa utalii wa Tanzania nchini Marekani, Macon Dunnagan kwa kuandika historia ya kupanda mlima Kilimanjaro zaidi ya mara 50.

Dunnagan mwenye umri wa miaka 63 aambaye amekuwa akiitangaza Tanzania kimataifa ni mtaalamu wa kuwasaidia wasafiri na mawakala wa usafiri katika kupanga likizo zao na kutembelea Tanzania Safari, kupanda mlima Kilimanjaro pamoja na Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushuka katika mlima huo kwenye safari yake ya mara ya 50 Dunnagan ametoa wito kwa watanzania na wageni kutoka sehemu mbalimbali kuwa na tabia ya kutembelea vivutio vilivyopo nchini na kujionea utajiri wa vivutio vya kipekee visivyopatikana sehemu nyingine duniani.

Advertisement

“Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi ikiwa ni pamoja na wanyama wa aina zote wakiwemo Simba Tembo Twiga na Chui pia kupanda Mlima Kilimanjaro,” alisema Dunnagan

Dunnagan alianza kupanda Mlima Kilimanjaro toka mwaka 1999.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini amesema serikali itaendelea kutambua michango ya watu wote wanaotangaza utalii wa nchi wa ndani na nje akiwemo Macon.

Aidha amesema kuwa Dunnagan alianza kuhamasika kupanda Mlima Kilimanjaro mwaka 1967 baada ya kuangalia movi ya “Snow of Kilimanjaro”.

1 comments

Comments are closed.