Apple kulipa kodi euro bil.13
IRELAND : KAMPUNI ya teknolojia nchini Marekani -Apple imetakiwa kulipa euro bilioni 13 ikiwa ni kodi ambayo haijalipwa kwa Ireland na Mahakama ya Haki ya Ulaya (ECJ).
Tume ya Umoja wa Ulaya ilishutumu Ireland kwa kuipa Apple faida zisizo halali za kodi miaka minane iliyopita lakini serikali ya Ireland imekuwa ikibishana mara kwa mara dhidi ya hitaji la kodi hiyo kulipwa.
“Mahakama ya Haki inatoa uamuzi wa mwisho katika suala hilo na inathibitisha uamuzi wa Tume ya Ulaya wa 2016: Ireland iliipa Apple msaada usio halali ambao Ireland inahitajika kurejeshewa,” mahakama ilisema.
Habari hizo zinawadia siku moja baada ya kampuni hiyo kubwa ya teknolojia kutoa aina yake mpya ya iPhone 16.
SOMA : Apple yapigwa faini kwa kukiuka sheria EU
Mpaka sasa Kampuni hiyo inadaiwa kiasi kisichopungua Euro bilioni 11 na dola za kimarekani bilioni 14 fedha ambazo zinatakiwa kulipwa.