Arsenal vs PSG: Nusu fainali ya kibabe

NUSU fainali ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya(UCL) inapigwa leo kati ya Arsenal na Paris Saint-Germain (PSG).

Mchezo huo wa kukata na shoka utafanyika uwanja wa Emirates jijini London, England ukiamuliwa na mwamuzi wa kati, Slavko Vincic wa Slovenia.

Kutinga hatua hiyo, Arsenal imeitoa bingwa mtetezi Real Madrid kwa jumla ya mabao 5-1 wakati PSG imeiong’oa Aston Villa kwa jumla ya mabao 5-4 hatua ya robo fainali.

Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya pili utafanyika Aprili 30 kati ya Barcelona na Inter Milan kwenye uwanja wa Olimpico Lluis Companys jijini Barcelona ukiamuliwa na Clement Turpin wa Ufaransa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button