TETESI za usajili zinasema Arsenal inapanga kuwasilisha ombi kwa ajili ya kuwasajili wachezaji wa AFC Bournemouth- beki wa kushoto wa Hungary, Milos Kerkez, 20, na winga wa Ghana, Antoine Semenyo, 24. (CaughtOffside)
Kocha wa Newcastle, Eddie Howe hana nia kuondoka klabu hiyo licha ya kuwa kwenye orodha ya makocha wanaohitajika kushika mikoba timu ya taifa England. (Telegraph – subscription required)
Barcelona na Real Madrid zote zina nia kumsajaili beki wa kushoto mhispania, Alvaro Fernandez, 21, ambaye Manchester United ilimuuza Benfica majira yaliyopita ya kiangazi. (Mirror)

Kiungo wa Manchester United na Denmark, Christian Eriksen, 32, anatarajiwa kujiunga na klabu yake ya zamani, Ajax wakati mkataba wake utakapofikia mwisho Old Trafford majira yajayo ya kiangazi. (Sun)
Everton inataka kumsajili winga wa Stuttgart na timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Silas Mvumpa, 26, Januari 2025. (Football Insider)
SOMA: Arsenal yaingilia usajili wa Nico Williams
Liverpool ina nia kumsajili wakati ujao beki wa kati wa klabu ya Palmeiras ya Brazil, Vitor Reis, 18.
Kinda huyo wa kimataifa wa Brazil ana kipengele cha kuachiwa cha pauni milioni 84. (Football Insider)
AC Milan inafikiria kumsajili winga wa Senegal anayekipiga Crystal Palace, Ismaila Sarr, 26, Januari 2025, ambaye amejiunga tu Agosti mwaka huu na klabu hiyo yenye makao yake makuu Selhurst Park. (Gazzetta dello Sport – in Italian)
Comments are closed.