“Arusha Mjini wajitokeze uchaguzi mitaa”

MSIMAMIZI wa uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini, John Kayombo ametoa rai kwa wanachi wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo kuanzia umri wa miaka 21 kujitokeza kuchukua fomu kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27.

Sambamba na hilo, wananchi hao wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la kujiandikisha daftari la wapiga kura ambalo litafanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu kwenye vituo vilivyopangwa.

Kayombo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha amesema hayo wakati akitoa maelekezo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mbele ya waandishi wa habari jijini Arusha.

SOMA: Vijiji 12333 kushiriki uchaguzi mitaa

Kwa mujibu wa Kayombo fomu za kugombea nafasi ya mwenyekiti wa kijiji, kitongoji na wajumbe wa halmashauri ya kijiji fomu zitatolewa na kutakiwa kurudishwa kuanzia Novemba Mosi hadi Novemba 7 mwaka huu kwa msimamizi wa uchaguzi.

“Uteuzi wa wagombea wote utafanyika Novemba 8 mwaka huu na muda kuweka pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea hao ni kuanzia Novemba 8 hadi 9 mwaka huu na uamuzi wa pingamizi utatolewa kuanzia Novemba 8 hadi 10 mwaka huu,” amesema.

SOMA: Takukuru yabaini harufu ya rushwa uchaguzi mitaa

Aidha amesema rufaa dhidi uamuzi kuhusu pingamizi la uteuzi zitapokelewa kuanzia Novemba 10 hadi 13 mwaka huu na kamati ya rufaa itatolewa kuanzia Novemba 10 hadi 13 mwaka huu.

Habari Zifananazo

Back to top button