Ashauri kulinda amani kwa maendeleo ya taifa

DODOMA: Katibu wa Kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia na ukatili kwa watoto nchini Tanzania (SMAUJATA ) Kanda ya Ziwa Mkoa, Agripina Msita, amewashauri Watanzania pamoja na vijana kudumisha amani ili nchi iweze kuendelea kupata maendeleo.

‎Akizungumza leo Juni 1, 2026 jijini Dodoma kuhusu umuhimu wa amani katika jamii, Msita amesema maendeleo yanapatikana katika mazingira yenye utulivu na mshikamano, akisisitiza kuwa sehemu yenye maendeleo ni sehemu inayompendeza Mungu.

‎“Naomba niwashauri Watanzania pamoja na vijana wenzangu kuwa kinachotakiwa ni kudumisha amani ili tuwe na maendeleo. Sehemu yenye maendeleo ni sehemu ya Mungu,” amesema Msita.

‎Aidha, ameeleza kuwa upendo ni msingi muhimu katika maisha ya kila siku, akifananisha mahusiano ya wananchi na yale ya mzazi kwa mtoto, ambapo kila hitaji hutimizwa kupitia upendo na mshikamano.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button