MSIMAMIZI wa uchaguzi wilayani Ngorongoro, Murtallah Mbillu amesema kuwa wilaya hiyo tangu zoezi la uandikishaji lilipoanza hadi kufikia jana wameandikisha wananchi 116,207 sawa na asilimia 95.9.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, Mbillu ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashuri ya Ngorongoro amesema zoezi hilo linaenda vizuri na mwitikio wa wananchi ni mkubwa.
SOMA: Waomba kusogezewa vituo kujiandikisha uchaguzi
Amesema ndani ya siku sita wamefanikiwa kundikisha wanaume 52,387 na wanawake ni 63,820 ambao jumla yake ni 116,207 sawa na asilimia 95.9.
Amesema jana wilaya hiyo imeandikisha wapigakura 7,520 ambao wanawake ni4,060 na wanaume ni 3,460
Amesema lengo ni kuandikisha wapgakura 121,139 huku akisisitiza zoezi hilo kwenda vema na hakuna dosari yoyote ilijitokeza huku mwamko wa wananchi ukiwa mkubwa