WAFANYABIASHARA wa soko la Manundu na watumiaji wa stendi ya Kijazi wilayani Korogwe wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batilda Buriani kuongezwa na kusogezewa karibu vituo vya uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura.
Ombi hilo limetolewa leo Oktoba 16, mara baada ya Mkuu wa Mkoa kufanya ziara ya kutembelea na kukagua hali ya uandikishaji katika wilaya hiyo.
Wakizungumza baadhi ya wafanyabiashara, Clement Nyangasa amesema kituo cha uandikishaji kipo mbali licha ya kuhamasika kushiriki zoezi hilo, hivyo ameomba kisogezwe karibu ili kuwapa nafasi wasiojiandikisha.
“Kwakweli tumehasika na zoezi hili lakini kituo kipo mbali na maeneo ya biashara zetu tunaomba kusogezewa karibu ili wanyabiashara wote waweze kujiandikisha,” amesema Nyangasa.
SOMA: Wachimbaji watakiwa kujiandikisha uchaguzi mitaa
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batlida Buriani amewahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wakazi Ili waweze kupata fursa ya kushirikisha kwenye kuchangua viongozi pamoja na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Comments are closed.