MKONGWE wa tenisi wa Marekani, Billie Jean King amependekeza kufanyika kwa mabadiliko makubwa ya sheria ili kuvutia zaidi hadhira ya vijana.
King amesisitiza kuwa lazima mchezo wa tenisi uwafikie watoto kuhakikisha unabaki kuwa moja ya michezo inayopendwa zaidi duniani.
SOMA: Novak Djokovic aanza kwa kishindo US Open
“Ningependa kuona majina na namba nyuma ya jezi za tenisi,” amesema King.
Pia amependekeza mabadiliko kwenye mfumo wa ufungaji utakaoondoa namba za zamani za 15, 30 na 50.
Badala yake King mwenye umri wa miaka 81 anaamini namba moja, mbili, tatu na nne zitafanya sheria kuwa rahisi na kusaidia watoto kuzielewa vizuri zaidi.
Amesema wachezaji wataweza kutambulika zaidi kwa mashabiki.
Imetafsiriwa kutoka Express