Novak Djokovic aanza kwa kishindo US Open

NYOTA wa tenisi Novak Djokovic ameanza jitihada zake za kutwaa taji la 25 la Grand Slam kwa ushindi dhidi ya Radu Albot katika raundi ya kwanza ya ubingwa wa US Open.

Mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa tenisi wa Arthur Ashe uliopo jiji la New York.

SOMA: Djokovic akemea vurugu Serbia

Taji moja zaidi litampa Djokovic rekodi ya pekee ya kuwa na mataji mengi zaidi ya Grand Slam kwa mchezaji mmoja mmoja katika historia.

Djokovic raia wa Serbia mwenye umri wa miaka 37 amemshinda Albot raia wa Moldova kwa seti 6-2 6-2 6-4 katika mchezo wake kwanza tangu alipotwaa medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki siku 23 zilizopita Paris, Ufaransa.

Sasa atakutana na mserbia mwenzake Laslo Djere katika raundi ya pili Agosti 28.

Habari Zifananazo

Back to top button