ATCL kuongeza safari, kujiendesha kwa tija

DODOMA — Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) litapanua wigo wa safari zake za kimataifa kwa lengo la kukuza biashara, utalii na uchumi wa taifa.

Akihutubia Bunge leo Juni 27, 2025, Rais Samia amesema safari mpya za ATCL zitajumuisha nchi za Nigeria, Msumbiji, Oman na Angola, hatua inayolenga kufungua fursa zaidi za kiuchumi na kuimarisha usafiri wa anga.

“Zamira yetu ni kuifanya ATCL kuimarika zaidi na kujiendesha kwa tija,” alisema Rais Samia mbele ya Bunge lililokuwa likifuatilia kwa makini.

Aidha, alieleza kuwa ununuzi wa ndege ya mizigo umeleta manufaa makubwa kwa wazalishaji wa ndani kwa kupunguza hasara waliokuwa wakiipata kutokana na changamoto ya usafirishaji wa bidhaa.

Rais Samia alisema hatua hiyo pia imesaidia kuitangaza Tanzania kitaifa na kimataifa kupitia huduma bora za usafiri wa anga na kuchochea mtengamano wa kibiashara baina ya Tanzania na nchi nyingine.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I am now making an extra $19k or more every month from home by doing a very simple and easy job online from home. sxs I have received exactly $20845 last month from this home job. Join now this job and start making extra cash online by following the instructions on the given website………………….. ­­W­­w­­w­­.­­J­­o­­i­­n­­S­­a­­l­­a­­r­­y.­­­C­­­o­­­m­­­

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button