ATCL yaongeza mapato

DODOMA: WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali imeongeza mapato kupitia Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kufuatia kuongezeka kwa idadi ya abiria wanaotumia huduma za shirika hilo.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Profesa Mbarawa alisema:

“ Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, ATCL imesafirisha jumla ya abiria 876,357, sawa na ongezeko la abiria 25,697 ikilinganishwa na 850,660 waliosafirishwa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2023/2024,” alisema Profesa  Mbarawa.

Aidha, alisema kuwa shirika hilo pia limesafirisha tani 5,869.81 za mizigo, ongezeko la tani 835.61 ikilinganishwa na tani 5,034.2 zilizosafirishwa mwaka uliopita.

Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa alisema kuwa wizara yake inaomba kuidhinishiwa zaidi ya Shilingi trilioni 2.74 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

 “Lengo letu ni kuboresha miundombinu ya anga, reli, bandari na barabara ili kuchochea uchumi na kurahisisha maisha ya wananchi,” alisisitiza Profesa Mbarawa.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button