Atupwa jela maisha kwa kumnajisi mtoto wake

MOROGORO: MAHAKAMA ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro imemhukumu Juma Mkandira ,44, mkazi wa kijiji cha Kitunduweta – Mhenda, kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kumnajisi mtoto wa kike wa kumzaa mwenye umri wa miaka saba (jina limehifadhiwa).

Juma alikamatwa Januari 18, 2025 katika kijiji cha Kitunduweta na kisha kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kilosa Februari 26, 2025 ili kujibu tuhuma zinazomkabili za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mtoto huyo.

Katika maamuzi ya kesi hiyo, mshitakiwa Juma alikiri kutenda kosa hilo mbele ya Hakimu Ageness Ringo.

Kwa kutenda kosa hilo, na alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kama adhabu huku ikielezwa kuwa hukumu hiyo inakusudia kuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

Hukumu hii imepokelewa kwa hisia mseto, huku jamii ikielezea matumaini kuwa hatua hii itasaidia kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na kuhamasisha wazazi na walezi kuwa macho kwa usalama wa watoto wao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button