Aukana uraia agombee urais 

ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya Credit Suisse, Tidjane Thiam ,62, ameukana uraia wake wa Ufaransa ili kutimiza masharti ya kushiriki katika uchaguzi wa urais wa Ivory Coast unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.

Mwaka 2023, Thiam alichaguliwa kuwa kiongozi wa PDCI, moja ya vyama vikuu vya upinzani huko nchini Ivory Coast na kumfanya kuwa mgombea wake.

Katika video iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook, Thiam amesema amewasilisha ombi la kurudisha hati yake ya kusafiria ya Ufaransa, ili kubaki kuwa raia wa Ivory Coast.

Advertisement

“Ninasisitiza upya ahadi yangu ya kufanya kazi kwa ajili ya mabadiliko ya kweli nchini Ivory Coast, ili hali ya maisha ya watu wa Ivory Coast iboreke. Hilo ndilo tunalopigania,” amesema Thiam.

Thiam amewahi kuwa Waziri nchini Ivory Coast chini ya Rais wa zamani Henri Konan Bedie, na aliondoka nchini humo baada ya kuondolewa madarakani kwa Bedie katika mapinduzi ya kijeshi ya 1999 na kufanya kazi katika kampuni ya ushauri ya McKinsey, na kampuni ya bima ya Aviva and Prudential, Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Credit Suisse mwaka 2015.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *