Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemteuwa Mhandisi Mbaraka Juma Ally kuwa Meneja Mkoa wa Dodoma wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).
Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Ally alikuwa RUWASA Mkoa wa Singida na anachukua nafasi ya Mhandisi Godfrey Kabula Mbabaye ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Uteuzi huo umefanyika ndani ya saa 12 baada ya ule wa Mbabaye kutenguliwa.