BAADA ya kukipiga na Al-hilal, Azam sasa watashuka dimbani Jumatano hii kukipiga na Esperance ya Tunisia kwenye mchezo wa pili wa kirafiki.
“Keshokutwa Jumatano saa 1.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Mchezo huo utafanyika jijini Tunis kwenye uwanja utakaotajwa hivi karibuni.” Imeeleza taarifa ya Azam.
Mchezo huo ni wa pili baada ya kuwafunga Al-Hilal ya Sudan mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa kirafiki.