Azam watoa pole waathirika mafuriko Hanang
KLABU ya Azam imeungana na Simba SC kuwapa pole ndugu walioguswa na vifo vya watu 49 waliokufa katika mafuriko yaliyotokea Wilaya ya Hanang mkoani Manyara jana.
“Tunatoa pole kwa familia za marehemu, ndugu jamaa na mafariki na Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi.”imeeleza taarifa yab klabu hiyo.
Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana wilayani humo yamesababisha vifo vya watu 49 na kujeruhi 85.