Bacca Kitasa cha makombe bara na visiwani

KAMA ulidhani upo kwenye kilele cha mafanikio basi embu mfikirie kwanza Mlinzi wa kati wa Yanga Ibrahim Hamad ‘Bacca’, moja ya nyota walioliteka soka la bongo kwa siku za hivi karibuni.

Nyota huyu wa Zamani wa KMKM sio tuu kwamba anafanya vizuri uwanjani bali ni mshindi wa medali za kutosha kwa kipindi kifupi.

Mwamba kutoka nchi ya Uchumi wa Bluu Zanzibar amebeba vikombe vyote kutoka ligi ya Zanzibar na Tanzania bara, akiwa KMKM , Bacca alishinda kombe la ligi kuu Zanzibar, kombe la shirikisho Zanzibar na ngao ya jamii, akafanya hivyohivyo Tanzania bara akiwa na Yanga hivyo ameshinda kila kombe Tanzania.

Bacca alijiunga na Yanga katikati ya msimu wa mwaka 2021/2022 hivyo akiwa KMKM na Yanga Bacca amevaa jumla ya medali Tisa, medali nane za ndani na moja ya michuano ya kimataifa ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x