Bajeti barabara MUHAS kutua bungeni, kamati yatoa maagizo

DAR ES SALAAM: KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeahidi kuwasilisha bungeni suala la ujenzi wa barabara zinazoingia na kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Kampasi ya Mloganzila ili itengwe bajeti maalumu kuboresha miundombinu hiyo.

Pia kamati imekiagiza chuo hicho kuhakikisha majengo mapya ya tiba yanayoendelea kujengwa Mloganzila yanapatiwa wataalamu stahiki mara tu yanapokamilika ili kuepuka kukaa muda mrefu bila kutumika ipasavyo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Husna Sekiboko ametoa ahadi na agizo hilo wakati kamati hiyo ilipotembelea miradi mipya ya hosteli, ukumbi wa mihadhara, maabara changamano, kantini, maktaba na ofisi za Tehama Machi 17 jana.

“Tumeshuhudia kazi nzuri, ila changamoto barabara zinazoingia na kutoka, lazima zipatiwe ufumbuzi ili kurahisisha namna watu watavyofika kupata huduma,” amesema Sekiboko.

Sekiboko amesema mradi huo unagharimu zaidi ya Sh bilioni 115, fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

Ameongeza kuwa mradi huo utaleta manufaa makubwa, ikiwemo kuongeza udahili wa wanafunzi, kuboresha mazingira ya kujifunzia, na kuongeza idadi ya madaktari ambao kwa sasa hawatoshelezi mahitaji yaliyopo.

Sambamba na hayo, Sekiboko amekipongeza chuo hicho kwa usimamizi mzuri wa mradi, akibainisha kuwa utekelezaji wake uko mbele kwa zaidi ya asilimia 10 ukilinganishwa na mkataba.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema Mkenda amefafanua kuwa Serikali imetenga Dola za Marekani 83 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali maalumu ya tiba katika kampasi hiyo.

Amesema hospitali hiyo itaongeza ufanisi wa kutoa mafunzo kwa vitendo, kufanya tafiti, na kuhudumia wagonjwa.

Aidha, amepongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa juhudi za kuendeleza Kampasi ya Mloganzila kuwa kitovu cha tiba.

Amesema kampasi hiyo itajumuisha vituo vya umahiri vitakavyotoa huduma za matibabu, elimu na utafiti kwa lengo la kuimarisha sekta ya afya pamoja na elimu ya juu nchini.


Amesisitiza kuwa lengo ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha taaluma za tiba katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, sambamba na kuzalisha wataalamu na wabobezi wa kutosha kuhudumia Watanzania pamoja na wageni wanaokuja kupata huduma za afya.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button